Unapoomba nitaje jina
Omba Mungu anikumbuke
Ni mnyonge mimi sina uwezo
Kwa maombi ntapata huru

Unapoomba omba kwa imani
Maombi atayasikia
Unapoomba uwe mnyenyekevu
Maombi atayajibu

Kulala kwetu kuamka kwetu
Kuishi kwetu ni neema
Tumaini letu ni kwako Bwana
Abudu ungama shukuru kwa dua zetu
Tumaini letu ni kwako Bwana

Unapoomba omba kwa imani
Maombi atayasikia
Unapoomba uwe mnyenyekevu
Maombi atayajibu

Mungu ajibu maombi maombi maombi
Mungu ajibu maombi maombi
Maombi ya watu wake
Uliza amani pokea shukuru
kulingana na ahadi zake ombi lako litajibiwa
Uliza amani pokea shukuru
kulingana na ahadi zake ombi lako litajibiwa

Unapoomba omba kwa imani
Maombi atayasikia
Unapoomba uwe mnyenyekevu
Maombi atayajibu

Song by The Saints Ministers