Unapoomba, nitaje Jina omba Mungu anikumbuke,
Ni mnyonge mimi sina uwezo, kwa maombi 'tapata nguvu

Unapoomba omba kwa Imani maombi atayasikia,
unapoomba uwe mnyenyekevu, maombi atayajibu

Kulala kwetu, kuamka kwetu, kuishi kwetu ni Neema,
tumaini letu li kwako Bwana, Abudu, ungama,
shukuru kwa dua zetu, tumaini letu li kwake Bwana

Mungu ajibu maombi maombi ya watu wake
Uliza, amini, pokea shukuru,
lingana ahadi zake ombi lako litajibiwa

Song by The Saints Ministers