Bwana hunificha mafichoni mwake
Hunifariji matesoni mwote
Nimepata mapumziko kwake Yesu
Hunilinda njiani pote

Hunificha mafichoni
Nionapo majaribu na mateso
Hunificha mafichoni
Bwana hunificha mafichoni mwake

Bwana hunificha mafichoni mwake
Ninalindwa naye utukufuni
Nimevikwa na mwangaza wa mwokozi
Ninafurahi siku zote

Hunificha mafichoni
Nionapo majaribu na mateso
Hunificha mafichoni
Bwana hunificha mafichoni mwake

Bwana hunificha mafichoni mwake
Mafichoni mwake hubarikiwa
Nimefunguliwa na Mkombozi wangu
Nani atakayenishinda

Hunificha mafichoni
Nionapo majaribu na mateso
Hunificha mafichoni

Bwana hunificha mafichoni mwake

Song by Elizabeth Nyambura