[In Swahili]

Unaona kama kila unachoguza kimeharibika
Ujasiri wa kusema tena umetoweaka
Maana kila unalosema wewe, kama unakosea
Umechanganyikiwa, ni Mungu anajua unayopotia
Na ukisema ueleze, wengi kwao ni furaha
Wewe umwombe Mungu, ubaki kimya
Na mengi umevumilia, moyo umenyong’onyea
Hapo ulipo sasa, ng’ang’ania tena

Bridge:
Na Mungu hajaruhusu, jaribu kuliko uwezo wako
Imani nusu, ongeza utashinda
Mungu hatoruhusu, ufe kabla ya baraka zako
Imani nusu, ongeza utashinda

Refrain:
Zipo nyakati za furaha, nawe utacheka tena
Usijali, Mungu yuko nawe
Zipo nyakati za furaha, nawe utacheka tena
Usijali, Mungu yuko nawe

Moyo wako una majeraha hufai
Tena unasubiri kauli ya mwisho ya mungu
Wapo wanaojua, we huna mtoto
Kwa kejeli wanaulizanga, “ana umri gani?”
Tena wanaojua, umefukuzwa kazi
Kwa kejeli wanaulizanga, “bosi wako yupo?”
Ila nakwambia, hayatodumu, ni nyakati tu
Hautobaki hapo, haya ni mapito
Jipe moyo tazama juu, mwombe Mugnu ujaisiri
Ni mapito tuu, jipe moyo mkuu
Japo nguvu ya kumwomba, muishie Mungu
Ni mapito tuu, jipe moyo mkuu

(Bridge + Refrain)

Repeat: Ni sawa hawajui, unakopita
Hata wakizusha maneno ya uongo wakakwambia umemuasi Mungu
Wakaja na unabii, wakasema umefika mwisho wako wewe
Wakainuka ndugu wa karibu, wakakusema ovyo ovyo
Ikawa kila kitu ni kimya, marafiki ni kimya
Kama ndoa ni yako, lakini ndani ni uadui

(Refrain)

Song by Goodluck Gozbert