Mungu, Elshadai wetu, matendo yako makuu,
umetukamilisha twajivunia (mifulizo) ya baraka zako
Twala, twanywa, twalala, twaamka,
uaminifu wako kwetu mkuu,
Hitaji letu tunalo
baraka zako zafululiza twashukuru kwazo
1. Hannah alibezwa kwa kukosa mtoto,
hakukataa tamaa, aliomba, wakati wa Mungu ulipofika
Samweli kazaliwa baraka nyumbani mwake
2. Waangalieni Ndege wa angani, hawapandi wala hawavuni,
hawakusanyi ghalani, ila Baba wa mbinguni huwalisha hao
Twala, twanywa, twalala, twaamka, uaminifu wako kwetu mkuu,
Hitaji letu tunalo baraka zako zafululiza twashukuru kwazo
Wengine walala hoi nawe wala na kusaaza wahitaji nini?
Mbona walilia cheo wengine hawana kazi, wahitaji nini?
Wengine wamelazwa na wewe una afya.. Mshukuru Mungu
Hesabu mibaraka moja moja, aogeleavyo papa baharini,
Mwanga wa jua hung'aa kote mvua ya masika hutunyea ilivyo baraka zake
Ilivyo nyota angani ndivyo baraka zake, Utukuzwe Mungu
Mungu, Elshadai wetu, matendo yako makuu,
umetukamilisha twajivunia (mifulizo) ya baraka
Song by The Saints Ministers