Nasifu Shani zako Elohim, safari mbali umenileta
Sina budi kuzishukuru hisani zako kuu
Kwa ukarimu wako nabarikiwa
nitatoa nini kwako Bwana na vyote ni vyako
miye ni mlinzi ulivyoagiza Edeni

Zangu zangu, Zangu zangu,
Zangu ni Shukrani Mungu

Sina neno uwapo karibu, nipatalolote si taabu,
Kifo na kaburi haviumi nitashinda kwako
Nilalapo nikuone wewe, gizani mote nimulikiwe
nuru za mbinguni kweli hazikomi,
Siku zangu zote, kaa nami Bwana

Zangu zangu, Zangu zangu,
Zangu ni Shukrani Mungu

Mapenzi yako sasa yatimie, wewe mfinyanzi mimi tope,
Unihojie dhambi zote, Unisafi Bwana
Natoa vitu vyote kwako leo, maisha, mali, moyo vipokee,
mwili wangu wote ni Hekalu lako, Niongozee Bwana, N'takuimbia

Zangu zangu, Zangu zangu,
Zangu ni Shukrani Mungu

Song by The Saints Ministers