[Swahili]

Watangoja sana
Wanaongoja kuanguka kwako
Wanaongoja kushindwa kwako
Wanaongoja umuache Yesu
Wanaongoja uharibikiwe wacheke

Waambie pole, pole pole
Ninaye Yesu, ninaye mwokozi
Waambie pole, pole pole
Watangoja sana

Yesu alipokufa akazikwa kaburini
Wengi walicheka sana Wengine walisema
“Si unajifanya ni mwana wa Mungu”
“Hebu jifufue tukuone”
Waliweka na walinzi walinde kaburi
Ili Yesu asifufuke
Waliweka na jiwe kubwa, pale kaburini
Ili Yesu asifufuke, Siku ya tatu ilipofika
Walinzi walishangaa, Yesu hayupo kaburini
Siku ya tatu ilipofika, Walinzi walishangaa
Yesu hayupo kaburini, amefufuka

watangoja sana
Wanaongoja matanga yako,
Wanaongoja urudiwe kwenyu nani wateleza
Wanaongoja ufutwe kazi wacheke

Waambie, pole, pole, pole
Ninaye yesu sibabaiki mimi nalindwa na Jehova
Ananipigia vita, Watangoja sana

Eh ni Mungu pekee yake
Analalamishwa juu yako
Hakuna silaha itainuka
Kinyume chako ifanikiwe
Maneno ya watu yasikuvunje moyo
Tegemea we utashinda, utashinda

watangoja sana
Wanaongoja kuanguka kwako
Wanaotaka ndoa yako ivunjike wacheke
Wanaotamani ufilisike wacheke
Wanaosema utakufa bila kuzaa mama

Waambie pole, pole, pole
Ninalindwa na jeshi la mbinguni
Wambie, pole, pole, pole
Watangoja sana

watangoja sana, Wanasema hutaolewa
Wanasema utashindwa na elimu
Wanaofitini ushukishwe cheo
Wanaosema huwezi fika popote

Waambie pole, pole pole
Wanaotabiri, wanaokuwazia
Watangoja sana
Ninaye Yesu, nasonga mbele
Nyuma sirudi tena
Watangoja sana

Song by Annastacia Mukabwa