[Swahili]

Nimehesabu na kuhesabu
Nimehesabu na kuhesabu
Nimeongeza na kutoa
Nikazidisha na kugawanya

Nimeona ni wewe
Yesu ni wewe tu
Hakuna mwingine
Yesu ni wewe tu

Pekee yako ni wewe
Yesu ni wewe tu
Hesabu zote nilizofanya
Nimeona ni wewe tu
Pekee yako ni wewe
Ni wewe Yesu ni wewe tu
Mwanzo mwisho ni wewe
Ni wewe Yesu ni wewe tu
Yesu ni wewe, ni wewe tu

Nikukumbuka ulikonitoa
Nikikumbuka ulionitendea
Ninakumbuka magonjwa ulioniponya
Ninakumbuka vita ulionipigania
Ninakumbuka safari umenitembeza
Ninakumbuka yale Mungu uliyotenda

Ninasema ni wee, ninasema ni wewe tu
Ni wewe, Yesu ni wewe, ni wewe tu

Nani awezaye kutenda uliyotenda Bwana
Nani angelipa garama ulionilipia
Kumbe si wenye mbio washindao michezo
Wala walio hodari washindao vitani
Nimeona watumwa wakipanda farasi eh Bwana
Wala si wenye hekima wapatao chakula
Bwana nimejumulisha, nikatoa nikagawa
Wewe sijaona mwingine eeh Bwana

Wewe Bwana, ni wee, ni wewe tu
Ni wewe, ni wewe tu

Song by Christina Shusho