Nifundishe kunyamaza
Nifundishe kunyamaza
Nisijejibu nikakukosea Mungu uu

Nifundishe kunyamaza
Nifundishe kunyamaza
Nisijejibu nikakukosea Mungu uu

We ewe Baba, wewe ni mwalimu mwema
We ewe Mungu wewe ni mwalimu mwema
Niko darasani kwako Masia
Baba naomba nifundishe kunyamaza

Niko katika kipindi hiki
Bwana naomba nifundishe kunyamaza
Natamani kunyamaza ah
Lakini si rahisi, nifundishe kunyamaza

Natamani kunyamaza Masia
Naomba nifundishe kunyamaza

Yapo mengi mambo yanayoweza
Fanya niseme
Yapo mazingira yanayoweza
Fanya nijibu nikakosea

Kwa maisha tunayoishi
Naomba nifundishe kunyamaza
Kwa ninayoyasikia kila siku
Bwana nifundishe kunyamaza

Kwa ninayoyaona kila siku
Eh Baba nifundishe kunyamaza

Mmmh mmmh wapo wanaoweza fanya
Nipambane eeh, nipambane
Yapo yanayoweza fanya
Nishindane eeh, nishindane

Bila neema ya kunyamaza
Naweza jikuta ninajibu vibaya
Bila neema ya kunyamaza
Naweza jikuta ninasema vibaya

Wee Yesu wewe
Naomba nifundishe kunyamaza
Wee Baba wewe
Naomba nifundishe kunyamaza

Kwa macho nimeona mengi
Naomba nifundishe kunyamaza
Kwa vinywa nimenenewa mengi
Naomba nifundishe kunyamaza

Kwa masikio nimesikia mengi
Bwana nifundishe kunyamaza

Oh nifundishe kunyamaza
Nifundishe kunyamaza
Nisijejibu nikakukosea Mungu uu

Nifundishe kunyamaza
Nifundishe kunyamaza
Nisijejibu nikakukosea Mungu uu

Eeh Baba nisaidie Baba
Ewe Mungu nisaidie Mungu

Ninatamana sana nijilinde
Nisije kukukosea
Ninachotaka nijilinde
Nisije kukupoteza

Watu wanaweza taka nipambane
Nikukose mwokozi
Wengi wanataka nipambane
Nikukose mwokozi

Kwa mazingira ninavyoyaona
Naweza pambana nikukosee
Kwa mwanadamu kunyamaza ni ujinga
Ninacholinda nisikukosee

Japo nitaonekana mpumbavu
Acha vyote vipite, nisikukosee
Japo yananichoma mpaka ndani ya moyo
Acha yapite, nisikukosee

Naweza pambana na wanadamu
Kumbe nikawa ninakupoteza Bwana
Naweza pambana na mwanadamu
Kumbe nikawa nakukosa Messiah

Naweza shindana na mtu
Kumbe nikawa nakukosa Messiah

Acha kwa watu niwe mjinga
Kwako niinuliwe
Acha kwa watu niwe mpumbavu sana
Kwako niwe shujaa

Acha kwa watu niwe kama mjinga
Kwako niwe mwenye hekima

Lakini sitaweza kunyamza
Bila kunifundisha
Maana kama mwanadamu inaniuma
Lakini mi naomba nifundishe

Maana kama mwanadamu inanitesa
Lakini mi naomba nifundishe kunyamaza

Bila kufundishwa nawe
Naweza nikapambana
Na katika kupambana kwangu
Nikakuta nakukosea

Nakuomba Baba, nakuomba
Nisaidie ninyamaze
Nakuomba Baba, nakuomba
Nisaidie ninyamaze

Hata wakiniona ni mjinga
Acha vyote nisikukosee
Japo wataniona ni mjinga
Kumbe ninalinda nisikukosee

Song by Martha Mwaipaja