[Swahili]

Verse 1:
Nafurahia mateso yangu, nafurahia mateso yangu
Ujapoharibika mwili huu, tapata mwingine kwa Baba
Ujapoharibika mwili huu, tapata mwingine kwa Baba

Chorus:
Nakaza mwendo, nifike Mbinguni
Nayakabidhi, maisha kwa Bwana
Nauone, uzuri wa bwana x2

Taabu na matatizo, hakuna
Kiu wala njaa, hakuna x2

Verse 2:
Lakini mji ule taa yake, ni mwana kondoo
Milele mji ule hauitaji, jua wala mwezi

Najua kuishi kwangu ni pigo, kufa ni faida

(Chorus)

Verse 3:
Lakini waongo na wazinzi, hawataingia
wala waabudu sanamu, hawataingia x2

Najua kuishi kwangu ni pigo, kufa ni faida

(Chorus)

Song by Rose Muhando