Neno la bwana ni upanga mkali unaokata pande zote
Wateule tusife moyo
Yeye yule aliyeanzisha kazi njema ndani yetu
Ameahidi atakamilisha
Kila siku ni kama jumapili (jumapili)
Kila siku kwangu, ni kama jumapili (jumapili) (2x)
Jumatatu kufunga na kuomba
Jumanne shiriki na wajane na yatima
Jumatano baba, chambua bibilia
Alhamisi, shiriki na wafungwa na wagojwa
Ijumaa baba kesha kanisani
(Kesha na kuomba)
Jumamosi(jumamosi)
Tangaza neno lako bwana yesu
Neno lako nahubiri
Kwa nyimbo zangu za injili
Kwa maana wewe ndiye mwamba
Imara na salama
(Nitangaze, nihubiri, nishiriki, nikusifu) (2x)
(Oh yahweh, yahweh) (3x)
Oh yahweh
Wateule tusiwe wakristo wa jumapili pekee
Siku zote za wiki tukamilishe injili
Na tutimize wajibu tuliopewa na yesu kristo
Watembelee wagonjwa hospitalini
Ushiriki na mayatima na wajane
Kuwasaidia wasiojiweza
Na kueneza injili hadi pande zote za dunia
Kutii amri zake mwenyezi mungu
Na kufuata maagizo yake
Tutii amri
Kila siku (jumapili) (2x)
Ah (jumapili (2x))

Song by Daddy Owen