Verse 1:
Kuna Mkono wa nguvu sana umetushikilia
Kama si Mungu wetu
Tungeangamia
Si kwa nguvu
Za majeshi yetu
Si ujasiri wetu
Tusisahau Kenya
Kule tulikotoka

Chorus:
Inua wimbo mpya
Wimbo wa shukurani
Kenya usisahau
Alikokutoa Bwana

Verse 2:
Inuka Kenya uangaze
Mwanga wa Mungu wako
Kwa maana mataifa yote
Yanakutazamia
Wakumbuke maskini wote
Yatima na wajane
Kenya utakatifu utakuinua

Chorus:
Inua wimbo mpya
Wimbo wa shukurani
Kenya usisahau
Alikokutoa Bwana

Bridge:
Tusizoe baraka zake Mungu Kenya
Tutizame taabu za mataifa mengi
Tusitese wakimbizi
Tusinyanyase masikini
Tujichunguze
Tujitakase
Tumtafute Mungu na kuomba

Song by Reuben Kigame And Sifa Voices